TThhaaammmeeess VViiieeewww IIIn nnfffaaanntttsssKuvalia sare za shule husaidia kujenda hisia ya...

9
1 TVIacademy.org Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG T T h h a a m m e e s s V V i i e e w w I I n n f f a a n n t t s s Muhtasari wa Chuo Nyote mkaribiwa na Wafanyakazi na Magavana wote kwenye Chuo chenye tamaduni anuwai na chenye kushinda tuzo. Ninaamini kwamba watoto wana nafasi moja tu kufaulu Shuleni na juhudi zangu zote kwa miaka 8 iliyopita kama Mwalimu Mkuu wa TVI zimekuwa kutimiza jambo hili: kuwapa watoto wetu – na familia zao - mwanzo bora maishani na elimu bora kwa Watoto wachanga iwezekanavyo. Tumefaulu pakubwa katika jambo hili: Elimu katika Thames View Infants imo ndani ya 20% bora ya shule zote kitaifa na kwa miaka kadhaa sasa, tumewekwa kama Shule ya Watoto Wachanga yenye mafanikio mengi zaidi katika Barking and Dagenham, pia kushinda shule nyingi zilizo katika mji London. DfE pia walituteua rasmi kama Kiongozi wa Kitaifa katika Shule ya Elimu na Usaidii wa Kitaalamu. Tulichaguliwa na Ofsted kama “Bora zaidi” mara mbili (mwaka wa 2009 na tena, mwaka wa 2014). Tunaamini kwamba tunaendelea kudumisha kiwango hiki. Mimi na wafanyakazi wangu tumejitolea kutumiza mahitaji yako wewe na familia yako. Tafadhali kuwa na uhakika kwaambatutajaribu kadri ya uwezo wetu kumpa mtoto wako hali bora ya mafunzo iwezekanavyo na kukupa huduma ya kipekee kama mteja na usaidizi kwa familia. Kiambatisho ni muhtasari wa taarifa muhimu sana kwako. Pamoja na usaidizi wako muhimu na malezi ya uangalifu, mtoto wako ataondoka Shuleni mwetu akiwa ameandaliwa vyema kwa Hatua inayofuata katika Elimu yake: Raia wa Uingereza – wenye uwezo, wajasiri, viongozi wa kesho, wenye upendo, wenye ufasaha na umantiki, wastahimilivu na mabingwa wa Kusoma na Kuandika na Hisabati. Paul Jordan, Mwalimu Mkuu. Maadili Yetu Hapa Thames View Infants tunjitahidi kuunda shule ya jamii inayojali, yenye furaha na usaidizi, ambayo kila mtoto na familia yake, kwa kweli ni muhimu sana. Tuntoa mazingira ya kusoma, ambayo kila mmoja anafikia uwezo wake kamili, haijalishi mwanzo wake. Tunawafunza watoto kuwaheshimu, kuwakubali na kuwathamini wanafunzi wenzao darasani na watu wazima katika jamii yetu ya shule yenye tamaduni amuwai na maishani mwao nje ya shule kwa kuwa watu wagwana. SWAHILI

Transcript of TThhaaammmeeess VViiieeewww IIIn nnfffaaanntttsssKuvalia sare za shule husaidia kujenda hisia ya...

1 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

TTThhhaaammmeeesss VVViiieeewww IIInnnfffaaannntttsss

Muhtasari wa Chuo

Nyote mkaribiwa na Wafanyakazi na Magavana wote kwenye Chuo chenye tamaduni anuwai na chenye kushinda tuzo. Ninaamini kwamba watoto wana nafasi moja tu kufaulu Shuleni na juhudi zangu zote kwa miaka 8 iliyopita kama Mwalimu Mkuu wa TVI zimekuwa kutimiza jambo hili: kuwapa watoto wetu – na familia zao - mwanzo bora maishani na elimu bora kwa Watoto wachanga iwezekanavyo. Tumefaulu pakubwa katika jambo hili: Elimu katika Thames View Infants imo ndani ya 20% bora ya shule zote kitaifa na kwa miaka kadhaa sasa, tumewekwa kama Shule ya Watoto Wachanga yenye mafanikio mengi zaidi katika Barking and Dagenham, pia kushinda shule nyingi zilizo katika mji London. DfE pia walituteua rasmi kama Kiongozi wa Kitaifa katika Shule ya Elimu na Usaidii wa Kitaalamu. Tulichaguliwa na Ofsted kama “Bora zaidi” mara mbili (mwaka wa 2009 na tena, mwaka wa 2014). Tunaamini kwamba tunaendelea kudumisha kiwango hiki. Mimi na wafanyakazi wangu tumejitolea kutumiza mahitaji yako wewe na familia yako. Tafadhali kuwa na uhakika kwaambatutajaribu kadri ya uwezo wetu kumpa mtoto wako hali bora ya mafunzo iwezekanavyo na kukupa huduma ya kipekee kama mteja na usaidizi kwa familia. Kiambatisho ni muhtasari wa taarifa muhimu sana kwako. Pamoja na usaidizi wako muhimu na malezi ya uangalifu, mtoto wako ataondoka Shuleni mwetu akiwa ameandaliwa vyema kwa Hatua inayofuata katika Elimu yake: Raia wa Uingereza – wenye uwezo, wajasiri, viongozi wa kesho, wenye upendo, wenye ufasaha na umantiki, wastahimilivu na mabingwa wa Kusoma na Kuandika na Hisabati. Paul Jordan, Mwalimu Mkuu.

Maadili Yetu

Hapa Thames View Infants tunjitahidi kuunda shule ya jamii inayojali, yenye furaha na usaidizi, ambayo kila mtoto na familia yake, kwa kweli ni muhimu sana.

Tuntoa mazingira ya kusoma, ambayo kila mmoja anafikia uwezo wake kamili, haijalishi mwanzo wake.

Tunawafunza watoto kuwaheshimu, kuwakubali na kuwathamini wanafunzi wenzao darasani na watu wazima katika jamii yetu ya shule yenye tamaduni amuwai na maishani mwao nje ya shule kwa kuwa watu wagwana.

SWAHILI

2 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

Tunataka watoto kufurahia muda wao shuleni na tumeunda mazingira salama na ya kuridhisha ambayo watahisi tunawajali na kuwathamini, kwa kukuza uhuru, ujasiri na uwezo wa watoto wa kujifanyia maamuzi yao.

Tunalenga kuifanya jamii yetu ya shule ya iwe ya kukaribisha ba ya kirafiki na tunahisi kwamba ni muhimu wazazi na walimu kushirikiana ili kuwasaidia watoto.

Kwa kuwa tunataka kusaidia familia zetu kupata thamani ya muda wanaotupatia, tunatoa huduma mbalimbali ambazo zinaongeza kila shule inaweza kufanya na siku ya shule.

Pia, tunafanya kazi kwa karibu na wataalam wote washirika muhimu walio

ndani ya mtaa na tunajivunia uhusiano wetu mzuri. Hii ni pamoja na Shule ya

Chini ya Thames, kituo cha Watoto cha Sue Bramley, The Chestnuts Nursery,

The Thames View Medical Centre, Sparrows Nursery (kilichojulikana hapo

awali Christchurch kama), Huduma kwa Jamii, shule za karibu na huduma za

elimu na usaidizi ndani ya Manispaa za London za Barking na Dagenham.

Pamoja tunatoa mtandao fanisi zaidi wa usaidizi kwa

familia na utoaji kamilifu wa “jiunge”.

Saa za Shule

Chekechea Miaka 3-4 Saa 2:45 asubuhi hadi 5:45 asubuhi

na saa 6:30 mchana hadi saa 9:30 mchana

Mapokezi Miaka 4-5 Saa 2:55 asubuhi hadi saa 5:45 asubuhi na saa 7:00 mchana hadi 9:15 mchana

Mwaka 1 na Mwaka 2

Miaka 5-6 Miaka 6-7

Saa 8:55 asubuhi hadi saa 6:15 mchana na saa 7:15 mchana hadi saa 9:15 mchana

Tafadhali jaribu kuhakikisha kwamba mtoto wako anawasili bila kuchelewa. Kila darasa huanza siku na somo la kusoma na kuandika au kuhesabu na mtoto wako atakosa mafunzo muhimu akichelewa.

Jaribu kuwasili dakik 5 kabla ya shule kuanza, kwani hutataka kusubiri kwa muda mrefu, haswa siku za baridi.

3 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

Tuna Breakfast Club kwa wazazi wanaofanya kazi wa watoto walio katika KS1, inayoanza saa 2:00 asubuhi, uandikishaji wa mwisho ukiwa 8:20 asubuhi. Watoto wanatunzwa na wafanyakazi wa shuleni. Kuna ada kidogo. Mwanzo wa mapema hauwafai watoto wote na ikiwa ungependa mtoto wako ahudhurie Breakfast Club, tafadhali njoo na uzungumze na Claire Smith, Naibu wangu kama Mwalimu Mkuu.

Ukichelewa, tafadhali usimwache mtoto wako nyumbani kwa siku nzima – ni

heri mtoto aje akiwa amechelewa kuliko kukosa kuja kabisa. Ukiwasili shuleni utahitaji kumwona wafanyakazi wa ofisi, ili kuhakikisha mahudhurio ya mtoto wako yanasajili na chajio kuagizwa.

Miradi ya Shule

Kama ‘shule pana’, tunawapa watoto vilabu mbalimbali vya shughuli za jioni, ambavyo wanafunzi huhudhuria bila malipo. Hivi ni pamoja na mfunzo ya ujuzi wa kandanda, densi na kompyuta. Vile vile, siku iliyorefushwa haiwafai watoto wote lakini tunajaribu kushirikisha matakwa ya kila mtu tunapolinganisha vilabu na mapendeleo.

Pia tuna Mshauri wa Usaidizi kwa Wazazi, anayeshughulikia vikundi

vya wazazi vya kila aina, na anaweza kutoa usaidizi kwa matatizo ya

kila siku yanayokumba familia. Njoo na ushiriki wasiwasi ambao

huenda ukawa nao kabla ya haujakuwa jambo kubwa.

Te Watoto wote wa Mwaka wa 2 wanaweza kuazima iPad au kushiriki katika Mpango Kununua Tena wa kujitolea. Shule yetu ina ‘utajiri mkubwa wa ICT’ na tumeshinda tuzo nyingi kufikia kiwango hiki. Watoto kote shuleni hutumia laptopu, iPads, Androids, Wiis/Xboxes na teknolojia zaidi za kisasa.

Meneja wetu wa Kiufundi atajibu maswali yoyote yanayohusu kompyuta uliyo nayo kuhusu kompyuta yako ya nyumbani. Njoo na uzungumze naye na atafanya kila awezalo kukusaidia.

Tunathamini “Wazazi kama Washirika” na mawasiliano mazuri kati ya nyumbani na shuleni ni muhimu. Kuna njia nyingi za kuwasiliana nasi au kujua kinachoendelea: Jambo la kwanza kufanya ni kupakua Proogramu yetu. Itakurusu: kutupa maoni yako kusoma blogu yetu kuangalia tarehe na matukio kutembelea tovuti ya shule kuwasiliana nasi saa zisizo za kazi kujisajili kwenye orodha yetu ya kupokea jarida la mtandaoni (na

usiwahi kukosa barua muhimu tena!)

4 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

Mimi na wafanyakazi hutuma ujumbe kwenye Twitter kila siku: ni njia bora nay a haraka kujua kinachoendelea Shuleni. Jisajili kwa mipasho yetu ya Twitter na ujue mengi zaidi:

@TVInfants (Paul Jordan, Mwalimu Mkuu) @ClaireTVI (Claire Smith, Naibu wa Mwalimu Mkuu) @Khaled_a_Ali (Khaled Ali, Mkuu wa EYFS) @TVI_MissCJones (Rosa Corcoran-Jones, Mwalimu Mkuu Msaidizi) @FiBashirTVI (Fi Bashir, Mtaalam wa Watoto na Familia) @TVI_ICTSupport (Simon Mordecai, Meneja wa ICT)

Tazama Kituo chetu cha “YouTube” … Thames View Infants TV (TVI TV). Kina zaidi ya video 250 za Podcast za Walimu na Vidokezo Bora vya mafunzo!

Huwa bora kukutana ‘ana kwa ana’ na walimu wetu, hasa wakati wa mazungumzo yanayohusu mafunzo. Hata hivyo, tunaelewa kwamba maisha ya wazazi yana shughuli nyingi na wakati mwingine ni vigumu kupata nafasi ya kuzungumza. Ikiwa wewe, au mtoto wako, ana swali kuhusu kazi ya ziada au anahitaji ushauri kuhusu kusoma nyumbani, unaweza kutuma barua pepe kwa:

[email protected] Walimu wetu watajaribu kujibu swali lako, au kupanga miadi kukusaidia zaidi wakati unaofaa.

Sare za Shule ni lazima kwenye Chuo chetu. Kuvalia sare za shule husaidia kujenda hisia ya kuwa umoja shuleni na kuweka hali ya mazingira bora ya kufanya kazi. Watoto huvalia shati la polo la shule, linalopatikana kwenye ofisi ya shule katika moja ya rangi 6 tofauti – nyeupe, kijani, manjano, rangi ya zambarau, rasiberi na rangi ya feruzi. Watoto wanaweza kuvalia rangi yoyote siku yoyote, lakini lazima wavalie shati la polo. Tuwie radhi, lakini wanafunzi hawaruhusiwi kuvalia mapambo ya vito shuleni.

Kwa kweli si jambo zuri kwa watoto kuja shuleni wakiwa wamevalia mavazi mengi wakati wa majira ya joto. Watoto wanacheza sana shuleni na kuvalia mavazi ya ziada yasiyohitajika (vesti, soksi ndefu, mashati na fulana) kutawafanya kuwa na joto jingi sana. Pia huongeza nafasi za vitu kupotea wanapozivua ili kupunga upepo. Tafadhali mvishe mtoto wako inavyofaa kulingana na hali ya hewa. Vile vile, tutawasaidia kuwa na afya (ikiwemo kuwawezesha kuvua nguo na kuvalia tena kukiwa na joto jingi na baridi nyingi).

Uhudhuriaji

Ni mahitaji ya kisheria kwamba watoto wanapaswa kuenda shuleni kila mara, na kwamba wazazi wao au wanaowatunza wanahakikisha jambo hili linatendeka. Kutohudhuria shule, isipokuwa kwa sababu ya ugonjwa, hakuruhusiwi.

5 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

Lazima likizo zote za familia zifanywe wakati wa likizo za shule zilizochapishwa. Shule haitatoa idhini kwa likizo zozote za familia wakati wa muhula. Wazazi watakaochukua likizo bila idhini au kuzidisha tarehe za kurejea watahatarisha:

Notisi ya Adhabu Moja (faini) kwa kila mtu mzima NA kwa kila mtoto (hata kama watoto wengine wanahudhuria shule tofauti).

Kupoteza nafasi ya mtoto wake ya shule.

Kujisajili upya na Mamlaka ya Ndani kwa nafasi mpya ya shule. Maelezo ya familia kufikishwa kwa Ofisa wa Mahudhurio wa Manispaa.

Lakini, ikiwa mtoto wako hataki kuja shuleni basi zungumza nasi. Huenda kukawa na sababu ya jambo hili na tutashirikiana kusaidia kutatua tatizo hili.

Uhudhuriaji wa kila mara na kuwasili bila kuchelewa ni muhimu sana ikiwa watoto wanahitaji kufaulu shuleni.

Ninapaswa kufanya nini mtoto wangu akiugua?

Ikiwa hali ya mtoto wako ni mbaya sana basi anapaswa kukaa nyumbani na augue kitandani.

Endapo hili litatokea, tunakuomba upige simu (020 8270 4317) au utume ujumbe wa maandishi (07943 922 655) kwenye ofisi ya shule kufikia saa 4 asubuhi kila siku ya kutokuwepo kwake na utuambie anavyoendelea. Tunafuata ushauri wa Serikali kuhusu afya na tutakupa ushauri pia.

Tunayo mazingira ya kujali na usaidizi, na tunaweza kumsaidia mtoto wako arejee shuleni mapema kwa njia nyingi:

Kumpa mtoto wako dawa (ukikamilisha fomu maalum kutoka ofisini)

'Kumtupia mtoto jicho' anapoendelea kupona na kukufahamisha 'jinsi anavyoendelea'.

Kuzungumza na madaktari katika Kituo cha karibu cha Matibabu cha Thames View.

Kumpa chagua ya vyakula mbadala (mpango maalum).

Kushirikiana nawe na mtoto wako ikiwa haponi au ikiwa unatatizika kumpeleka shuleni kila asubuhi.

Kuwasaidia kufuatilia kile ambacho amekikosa.

6 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

Je, "uhudhuriaji mzuri" ni nini? Kwa sababu inweza kudhuru elimu ya mtoto asipokuja shuleni kila mara, Serikali imewekea shule zote Lengo la Kitaifa la Uhudhuriaji wa Shule, ambalo ni kwamba wanafunzi wahudhurie kwa asilimia 95 ya vipindi vyote.

Hii inamaanisha kwamba, kwa mwaka mzima, wanafunzi wakose shule tu kwa wastani wa siku 1 ya shule kwa mwezi (siku nusu baada ya wiki mbili). Tuna bahati sana, kwa sababu ni nadra sana watoto kukosa kuhudhuria shule katika shule yetu.

Katika Thames View Infants tayari watoto wengi huhudhuria shule kila siku na uhudhuriaji wao ni wa asilimia 100.

Kila muhula tunazituza familia zetu zote zinazotimiza Uhudhuriaji wa asilimia 100 na “Shada la Maua” maalum na maarufu.

Pia tunamtuza baiskeli mtoto ambaye ameonyesha uimarikaji bora katika uhudhuriaji wake kwa mwaka mzima hadi leo.

Nitajuaje mahudhurio ya mtoto wangu? Tunashirikiana na familia zetu na, kama shule, tunafuatilia uhudhiriaji kila mara. Mara nyingi, utakuwa tayari unajua ikiwa uhudhuriaji wa mtoto umepungua kwa sababu wakati mwingine, tutakuwa tumeuzunguzia pamoja. Kwa kawaida, kila baada ya wiki mbili, tunachunguza rasmi uhudhuriaji wa watoto wetu. Kila muhula, tunamtumia kila mzazi batua ikiwa uhudhuriaji wa mtoto wake utakuwa chini ya vigezo vinavyofuata:

Asilimia 100% (hajawahi kukosa kuenda shuleni) Asilimia 97% ( kukosa kuenda shuleni karibu siku

nusu kwa mwezi) Chini ya asilimia 95 (kukosa kuenda shuleni siku

nusu kwa wiki mbili Chini ya asilimia 90 (siku nusu kwa wiki) Chini ya asilimia (karibu siku moja kwa wiki) Chini ya asilimia 75 (karibu siku moja na nusu

kwa wiki)

Ingawa uhudhuriaji nwa ‘asilimia 90' unaonekana kuwa wa juu, kwa amali ya elimu ya mtoto, asilimia 10 aliyokosa kuenda shuleni inaweza kuchangia mwaka mzima wa shule. Kwa kukuarifu kupitia barua, tunaweza kufanya kazi pamoja ili kusaidia kuimarisha uhudhuriaji na mafanikio ya mtoto wako kama mwanafuzi.

7 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

Athari za mahudhurio ya kiwango cha chini ni gani?

Kutohudhuria shule kila mara kunaweza kuwa na matokeo mabaya kwenye elimu ya mtoto. Kitakwimu, ni watoto walio na zaidi ya asilimia 90 ya mahudhurio wanaopata alama bora za mtihani na wana uwezekano mkubwa wa kupata kazi nzuri siku za usoni.

Watoto ambao mahudhurio yao ni mabaya wana tatizo la kujumuishwa katika maisha ya shule na huwa matatizo kuwa na marafiki.

Watoto huwa na ugumu zaidi 'kufuatilia' kile ambacho wamekosa wakikosa kuwa shuleni kila mara.

Mara nyingi, ni watoto wanaokosa kuwa shuleni kila mara ambao mara nyingi huzingatiwa kuwa hatarini sana.

Academy Trust hii hushirikiana kwa karibu na Mamkala ya Ndani ya Manispaa za mji wa London za Barking na Dagenham, ambao watashtaki familia zinazokosa kuhakikisha mtoto wao anahudhuria shule kila mara, kwani ni hatia. Wazazi/walezi wako katika hatari ya kutozwa faini, au kufikishwa mahakamani, kulazimika kuhudhuria madarasa ya uzazi au kufungwa jela kutokana na kesi nyingi mbaya. Hatutaki jambo hili kutendeka kwa familia yoyote ya mwanafunzi wa Thames View Infants.

Shule yetu ni mazingira yanayojali na yenye furaha, na orodha yake ndefu ya kusubiri, basi pia si vyema kwa familia hizo zinazotaka kumleta mtoto wao shuleni mwetu, lakini haziwezi kwa sababu hakuna nafasi.

Mipango ya Usajili

Tuna idadi kamili za nafasi katika kila kikundi cha mwaka. Thames View Infants hufuatilia mipango ya usajili iliyokubaliwa na Manispaa za mji wa London za Barking na Dagenham. Ikiwa hakuna maombi zaidi ya nafasi shuleni kuliko idadi inayoweza kusajili, basi Mamlaka ya Ndani inaweza kuwasajili watoto wote wanaohitaji nafasi. Wakati kuna maombi zaidi kuliko nafasi, basi Mamlaka ya Ndani inahitaji vigezo vya usajili vya kuamua ni nani atapewa nafasi na nani hatapewa. Vigezo vya usajili ni kama vifuatavyo:

8 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG

1. "Watoto Wanaotunzwa". 2. Watoto walio na kaka au dada anayehudhuria shule hiyo au Shule ya Kiwango cha

Chini ya Thames View. 3. Watoto wanaoishi karibu na shule kwa kupimwa kwa njia ya kutembea iliyo karibu.

Watoto wasiopewa nafasi majina yao yataandikwa kwenye orodha ya kusubiri nafasi.

Taratibu za Malalamiko

Tunajitahidi kuwapa watoto wetu wote elimu bora. Mwalimu Mkuu na wafanyakazi wanatia bidii sana kujenga uhusiano mwema na wazazi wote. Hata hivyo, Thames View Infants, kama Chuo, inahitajika kisheria kuwa na, na kuchapisha utaratibu wao wa malalamishi. Mara kwa mara wazazi na walezi watakuwa na matatizo ya kawaida na halali kuhusu maendeleo, mafanikio, tabia au maslahi ya watoto wao, au kuhusu masuala mengine yanayohusiana na shule. Kutoelewana kwingi mara nyingi huwa si makusudi na walimu wetu watakusikiliza na kufanya kila wawezalo kutatua tatizo. Wakati mwingi, huwa ni vizuri kuwasilisha tatizo au shida moja kwa moja kwa mwalimu wa mtoto; hata hivyo, kulingana na hali ya malalamiko, huenda ukahitaji kuwasilisha tatizo moja kwa moja mwa Mwalimu Mkuu – ambaye, kulingana na hali ya tukio, atashughulikia tatizo kwa njia rasmi au isiyo rasmi. Malalamiko yanashughulikiwa kupitia Mchakato wa hatua 4, ambazo zinaweza kutazamwa kikamilifu hapa: http://is.gd/I9bK7f

Sera ya Kanuni za Maadili na Ulinzi

Tunafuata Miongozo mbalimbali ili kutimiza wajibu wetu wa Kisheria ili kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaendelea kuwa Salama na kutunzwa vyema. Wakati mwingine, tunalazimika kushiriki taarifa na Huduma za Jamii au Afisa Aliyeteuliwa wa Malaka ya Ndani (kwa Ulinzi wa Watoto) na kuomba ushauri au mwongozo wao. Pia sote tuna wajibu wa kutunza na jukumu la kuonyesha tabia njema na kwa kitaalam tukiwa kwenye Jengo la Shule. Kufanya hivyo, kunachangia kuwepo kwa uhusiano mwema wa kufanya kazi, ambao, watoto wanajitahidi na kunawiri. Nakala ya Sera yetu ya Kanuni za Maadili inaonyeshwa ndani ya Ofisi ya Shule yetu. Tunatumaini kwamba taarifa hii itakusaidia. Hata hivyo, inakuambia tu kuhusu badhi ya mambo tunayofanya shuleni mwetu – kwa hivyo tafadhali njoo katika Ofisi ya shule na uulize kitu chochote kingine unachotaka kujua, kama vile kahawa yetu ya asubuhi, jinsi ya kupata jarida letu kwa njia ya barua pepe … au kusema tu hujambo! Taarifa na rasilimali zaidi zinapatikana kwenye tovuti ya shule yetu:

TVIacademy.org

9 TVIacademy.org

Thames View Infants: kampuni yenye dhima ya dhamana Imesajiliwa Uingereza: Nambari ya Kampuni: 08163191 Ofisi Iliyosajiliwa: Thames View Infants, Bastable Avenue, Barking, Essex IG11 0LG